Hazina

Kila siku Radio Kicheko Live inarusha vipindi 10, taarifa za habari 3, habari kwa ufupi mara 2, na makala 2 za habari. Asilimia 80 ya maudhui hayo ni ya kuelimisha jamii katika mambo mbalimbali yanayogusa maisha yao ya kila siku.
Tumesikia maoni ya wasikilizaji wetu ambao wameomba waweze kusikiliza baadhi ya vipindi baada ya kuruka hewani kwani mara nyingi vinaporuka wanakuwa katika majukumu mengine.
Kupitia ukurasa huu wa Hazina ya vipindi, Radio Kicheko Live itaweka baadhi ya vipindi kwa mwezi mmoja baada ya kuruka ili wasikilizaji waweze kusikiliza kwa wakati wanaopenda.
Karibuni Sana!

Featured shows

View all shows

Bima BUMACO na Maendeleo ni kipindi kinachodhaminiwa na kampuni ya bima ya BUMACO chenye lengo la kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa bima, aina za bima, masharti, majanga na utaratibu wa kudai fidia janga linapotokea.

Fahamu Elimika

Fahamu Elimika ni kipindi chenye lengo la kutoa elimu kuhusu mambo mbali mbali yanayogusa maisha ya kila siku ya msikilizaji katika nyanja mbalimbali. Vipindi hivi vinaweza kusikilizwa na Wadau wa Radio Kicheko tu. Kama unapenda kuwa Mdau wa Radio Kicheko tafadhali jisajili kwa kubofya "Register".

Latest episodes

Subscribe

Recent posts